Aiyola - Harmonize

Play the audio for 'Aiyola'

Aiyoo aiyoola iyeeh
Ayolaa mamaaa! 
Aiyoo aiyoola iyeeh 
Nilifundishwa na bibi kijijini jinsi ya kupenda 
Na mwanamke hapigwi na ngumi ila upande wa kanga
Tena mapenzi sio league, nikakubali kushindwa 
Mi sikufunzwa graji, tushindane risasi kwa panga 
Mbona nilikudhamini mengi nikakusevia
Sitosema hadharani wengi wakayasikia
Sio wakunipanda kichwani, hukumbuki tulipotokea
Na kunishusha thamani, kipi nilichokosea
Ingawa kidogo nilichopata, nikajinyima uridhike
Ila hukujali ukanikatili moyoo 
Majirani walinicheka uliponiforce nipikee, ahhh sio siri ilinivunja moyoo
Kisirani, ugomvi bila chanzo, ni ukweli uko moyoni sina budi nilivue pendo 
Ingawa kishingo upande

  (CHORUS)
Aiyooo aiyoola iyehhh, sitaforce unipende
Aiyooo aiyoola iyheeeh, ila kishingo upande mama
Aiyoo aiyolaaaa iyehhh, basi bora uende mama
Aiyoo aiyoola iyehhh ×2

Sitosema mapenzi basi nimeumbwa na moyo
Moyo wenye matamanio na unapenda pia
Ila nitaijuitia nafsi nilikufanya chaguo, ahhh chaguo la moyo kumbe ulipita njia
Nilivyowanyima ndugu visiri nikakutunzia usijeleta vurugu akili ukaitibua
Najuta kujitia bubuu, sitaki vya kusikia kisa pendo unisurubu mengi nishayafumbia
Mbona nilikuthamini mengi nikakusevia sitosema hadharani wengi wakayasikia
Sio wakunipanda kichwani, hukumbuki tulipotokea
Na kunishusha thamani, kipi nilichokosea
Kisirani, ugomvi bila chanzo, ni ukweli upo moyoni sina budi nilivue pendo ingawa kishingo upande

  (CHORUS)

Check out all songs from 'Harmonize (Singles)' Album

Album Lyrics

pinteresttwitterfacebookgoogle-plus